Mark 1:1-6

Mahubiri Ya Yahya Mbatizaji

(Mathayo 3:1-12; Luka 3:1-8; Yohana 1:19-28)

1 aMwanzo wa Injili ya Isa Al-Masihi, Mwana wa Mungu.

2 bKama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Tazama, nitamtuma mjumbe wangu mbele yako,
atakayetengeneza njia mbele yako”:

3 c“sauti ya mtu aliaye nyikani.
‘Itengenezeni njia ya Bwana,
yanyoosheni mapito yake.’ ”

4 dYahya alikuja, akibatiza huko nyikani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi. 5 eWatu kutoka Uyahudi wote na sehemu zote za Yerusalemu walikuwa wakimwendea. Nao wakaziungama dhambi zao, akawabatiza katika Mto Yordani. 6 fYahya alivaa mavazi yaliyotengenezwa kwa singa za ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu.
Copyright information for SwhKC